Mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu Jimi Wanjigi amesema kwamba yeye ndiye risasi ya mwisho itakayo faulu kumtuma Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga nyumbani.
Wanjigi ambaye amekuwa akifadhili kampeni za Raila katika miaka za hapo awali, ameonyesha matumaini ya kukitwaa kiti cha urais iwapo atapeperisha bendera ya ODM katika uchaguzi mkuu ujao.
"Sio siri sasa kwamba Baba na wengine wamekuwa wakisema kwamba yuko na risasi ya mwisho. Hiyo risasi iko hapa Homa Bay leo na nyinyi na hiyo risasi ni mimi." Alisema Wanjigi baada ya kukutana na waakilishi wa ODM kutoka kaunti ndogo nane za Homa Bay katika mkahawa mmoja.
Pia soma
Magazeti Ijumaa: Rais Uhuru na DP Ruto Walitumiana Jumbe za Makasiriko
"Nawatakia mema watu wa Homa Bay na chama chetu cha ODM, sisi tunataka kupata uongozi na hiyo ndio sababu vyama huundwa." Alisema mwanasiasa huyo.
Wanjigi alitoa wito kwa chama cha ODM kumpatia nafasi ya kukiongoza huku akiwahidi ufanisi kutokana na uongozi wake.
Ziara hiyo ya Wanjigi inatazamiwa kifika kilele Jumapili hii huku akiwa amezuru kaunti zote za mkoa wa nyanza.
Kupitia kwa kauli mbiu yake ya "Fagia wote', Wanjigi ana matumaini ya kutembea pembe zote nchini kujitafutia umaarufu.
"Tunataka kuwatoa wote kwa sababu ni wao ndio chanzo cha matatizo yanayotukumba wananchi." Alisema Wanjigi.
Kiongozi huyo amekashifu uongozi na sera mbaya za uongozi wa serikali ya Jubilee na kusema kwamba taifa linahitaji mwamko mpya ili kufufua uchumi na kuleta matumaini kwa Wakenya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke
Pia soma
William Kabogo Asisitiza Lazima Awe Debeni Kuwania Urais 2022 Itakapofika
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4N2fZdmpKKlmWK7pbXOZqmiq5Gotm7FwGaksKGjnbxuxcBmqZqhnJZ6or%2FEpphmopmitm7DwKehop%2BZYq6stdaaZLOhkaeur7WMp7CapqqWe6nAzKU%3D